SWAHILI MICROSITE

swahili-house-banner

KARIBU KAMPUNI YA MAWAKILI YA YAKUBU
Sisi ni Kampuni hodari na makini ya uwakili, tunafanyia shughuli katika Jiji la kihistoria la Dar-es-Salaam, Tanzania. Wateja wetu wanatambua na kufurahia huduma zetu adhimu tunazowapa kwa umakini na ustadi mkubwa.

Uaminifu na uzingatiaji taaluma huhuisha mahusiano kati yetu na wateja wa ndani na nje ya nchi. Tumefanikiwa kuaminiwa na wateja wetu wa Tanzania na nje ya mipaka yake. Tumejidhatiti kuhudumia kwa kuzingatia Maadili, gharama nafuu na ubora wa hali ya juu kabisa.

Ubunifu na Ubora
Kampuni yetu inaendana na wimbi la mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea Tanzania na Bara zima la Africa. Tumewekeza kwa kiasi kikubwa kwa wataalum mahiri na nguli. Kwakufanya hivyo, imetuwezesha kutoa huduma za kisheria katika maeneo magumu  zaidi.

UTAMADUNI WA KAMPUNI
Asili ya Jiji la Dar-es-Salaam inatoka na urithi maridhawa kutokana na biashara za asilia na za ng’ambo kupitia baharini. Kwa maana hiyi na ufahamu huo wa kibiashara, ndivyo vinanyoendelea kutuhuisha katika utendaji wetu. Tumelinasibisha jambo hili kwa kuzingatia uswa kwa viwango vya juu kabisa vya maadili katika kila eneo tunalotoa huduma.

NINI TUNAFANYA
Kutokana na ubora wa kazi zetu, Makampuni makubwa ya biashara, makampuni ya sheria ya kimataifa na watu wa hadhi za juu wamechagua kuhudumiwa na timu yetu ya Ushauri kuwahudumia katika maeneo yafuatayo;

 • Mafuta na Gesi (Mikondo ya juu, kati na chini kabisa)
 • Ushirikiano kati ya Sekta Binafsi na za Umma
 • Majadiliano ya Kibiashara
 • Mashauri ya Kifedha
 • Uchimbaji madini
 • Majengo, Makazi, Viwanja na Ardhi
 • Ufuatiliaji na Ukusanyaji Madeni
 • Huduma za Kibenki
 • Ushauri wa Bima
 • Uendeshaji Miundombinu ya Miradi na
 • Ushauri wa Kodi